AfyaHabariNews

Serikali yatakiwa kuwekeza kwenye sekta ya afya kukabiliana na ongezeko la matatizo ya afya ya kiakili

Changamoto imetolewa kwa serikali kuboresha huduma katika taasisi za afya kukabiliana na ongezeko la watu wanaokumbwa na matatizo ya afya ya akili.

Mtaalamu wa afya ya akili, Kadzo Rubene Alibainisha Kuwa asilimia kubwa ya Wakenya wako katika hatari kubwa ya kukumbwa na tatizo hilo.

Alisema watu wengi wanapofika kwenye taasis za afya hukosa kufanyiwa ukaguzi wa kina kuhusu chanagamoto za kiakili.

Kulingana na Kadzo ni kwamba chanagamoto za maisha na majanga ni miongoni mwa sababu kuu ambazo zimepelekea idadi kubwa ya watu kujipata katika hali hiyo.

“…. Mwanzo tukisema environment tunamaanisha kama hali ya Uchumi, hali ya uchumi ikiwa mbaya na yule mtu mtu labda anafaa kuhakikisha kuwa familia au watu ambao wako karibu naye wanapata chakula na vitu vingine vya msingi na hawezi kujimudu kimaisha, hiyo inaweza enda ikamfanya mtu akwa na matatizo ya kiakili.” Alisema Kadzo.

Upande mwingine mtaalamu Nancy Anyona alidai kwamba asilimia kubwa ya watu wanaotembelea vituo vya afya hupatikana na tatizo hilo.

Ameonya alionya kwamba endapo hatua za haraka hazitachukuliwa Wakenya wengi zaidi watazidi kuathirika na tatizo hilo.

“Kati ya watu 6 ambao wanaenda kuvisit kituo cha afya, ile unatoka nyumbani eti nainda hospitali kwa sababu sisikii vizuri 6 of them wanapatikana wako na tatizo la afya ya kiakili,” alieleza Anyona.

Kulingana na takwimu mtaalamu huyo liongeza kuwa Kenya imeshikilia nafasi ya 4 Barani Afrika na ya 9 kwa watu wanaokabiliwa na tatizo hilo.

BY MAHMOOD MWANDUKA