HabariNews

Wizara ya elimu yatangaza marekebisho ya tarehe ya likizo fupi nchini

Serikali imetangaza mnamo Mei 29, 2024 tarehe mpya za likizo fupi kwenye muhula huu wa pili.

Katika taarifa yake ya marekebisho ya tarehe za hapo awali, wizara ya elimu kupitia katibu Belio Kipsang ilieza kwamba marekebisho hayo yaliafikiwa ili kufidia muda uliopotea kutoka na mafuriko na mvua kubwa.

Wizara hiyo ilibaini kwamba wawanafunzi wa chekechea, shule za msingi na zile za sekondari watafunga shule kwa ajili ya likizo fupi kutoka Juni 26-28, 2024, Kipsang akiwataka wakurugenzi wa elimu kaunti zote nchini kuwasilisha taarifa hiyo kwa wakuu wa shule katika maeneo yao.

“Mabadiliko hayo yanawezapelekea mabadiliko katika shughuli zilizopangwa na ratiba. Kwa hivyo mnaagizwa kuwasilisha maudhui ya kikao hiki kwa walimu wakuu wa shule zote katika maeneo yenu.” Alisema Kipsang.

Hata hivyo wanafunzi wa shule za upili za za mabweni wameratibiwa kurudi shuleni kufikia Juni 30, 2024.

Kulingana na kalenda ya awali wanafunzi waliratibiwa kufunga kwa likizo hiyo Juni 20- 23 mwaka huu.

Awali shule zote zilifaa kufunguliwa Aprili 29 kwa muhula wa pili lakini tarehe iyo ilipelekwa mbele hadi Mei 6 na baadaye kupelekwa mbele tena hadi Mei 13 baada ya idara ya utabiri wa hali ya anga kutabiri kupungua kwa kipindi cha mvua nyingi.

BY MAHMOOD MWANDUKA