HabariNews

Wanasiasa Pwani wakashifiwa kwa kusalia kimya kwenye mjadala tata wa muguka

Mashirika ya utetezi wa haki za Kibindamu yameeleza wasiwasi wao kwa viongozi katika ukanda wa pwani kusalia kimya kuhusu mjadala wa muguka unaoendelea nchini.

Mashirika ya MUHURI, KEMWA na HURIA ni ya hivi punde kujitokeza na kutangaza kuunga mkono marufuku dhidi ya bidhaa hiyo.

Wakizungumza siku ya Ijumaa Mei 31, 2024 mashirika hayo yalitaja mjadala wa muguka kuwa mjadala wa kitaifa wakionyesha kushangazwa na viongozi kama wkama vile gavana wa Lamu Issa Timamy, mbunge wa Nyali miongoni mwa wengine.

Kulingana na mashirika hayo muguka ni bidhaa ambayo imetambuliwa kuwa na sumu ambayo ni hatari kwa watumizi wakiwataka viongozi wa kisiasa Kutangaza misimamo yao kwenye suala hilo.

“Wanasaiasa wanafanya nini katika eneo hhili la Pwani? Muhamed Ali uko wapi hatukuoni tunataka kusikia msimamo wako kuhusu hili suala.

Hassan Sarai uko wapi? Tunataka kukuona, tunataka kukusikia. Huu sio mjadala kuhusu Kilifi, Kwale na Mombasa, huu ni mjadala wa kitaifa, huu ni mjadala ambao ni lazima ulete pamoja wanasiasa wote,” yalisema mashirika hayo.

Yaliongeza kwamba kaunti ya Lamu ndilo eneo ambalo kuna watumizi wengi wa muguka wakieleza haja kwa viongozi wa kisiasa ukanda wa pwani kuongea kwa kauli moja ili kufanikisha vita hivyo.

“Lamu ndio mwanzo watu huko watu wanatumia sana hii mugokaa, Taita taveta wanatumia, kwa nini hatusikii kitu chochote kutoka kwa gavana wa Lamu kuhusu mjadala huu? Tunataka kusikia na hatutaki kusikia mgawanyiko wa maoni kuhusu hili suala.” Yaliongeza mashirika hayo.

Zaidi ya hayo mashirika hayo yalipongeza hatua iliyochukuliwa na magavana katika kaunti za Mombasa, Kilifi na Tiata Taveta kusimama na kupiga marufuku bidhaa hiyo.

“Napenda kuchukuwa nafasi hii kwanza kumpongeza wetu Abdulswamad kwa kazi aliyoifanya si kazi mbaya ni kazi nzuri kwa jamiii yote ya Kenya…. tunahimiza serikali ya kaunti ya Mombasa, Kilifi na Taita Taveta kusimama kidete katika vita dhidi ya utumizi mihadarati…,” yalikariri mashirika hayo.

Haya yanajiri huku Vuta nikuvute ikiwa imeshuhudiwa kati ya maafisa wa trafik katika mipaka ya kaunti zilizopiga marufuku bidhaa hiyo.

Mjadala unaendelea kuchukuwa mkondo tofauti kufuatia hatua ya wadau mbalimbali, wananchi na badhi ya viongzozi kutoka pande zote mbili kuonyesha misimamo mikali.

Awali rais William Ruto alikutana na viongzo kutoka Embu kujadili marufuku hiyo na kubaini kwamba muguka ni mmea ambao ni halali nchini kauli iliyokashifiwa na viongozi mbalimbali ukandaw a pwani.

Hata hivyo rais alimuagiza wazri wa kilimo kuandaa kikao na viongozi kaunti za pwani zilizopiga marufuku bidhaa hiyo mkutano ambao unatarajiwa kufanyika jumatatu ya Juni 3, 2024 kutafuta suluhu ya kudumu kwenye suala hilo tata.

Unaweza soma pia:

https://sautiyapwanifm.com/2024/05/28/mahakama-ya-embu-yaondoa-marufuku-ya-muguka-mombasa-kilifi-na-taita-taveta-kwa-muda/

https://sautiyapwanifm.com/2024/05/28/gavana-wa-kwale-akaidi-wito-wa-wenzake-na-kukataa-kupiga-marufuku-muguka/

BY EDITORIAL DESK