HabariNews

Muungano wa KMPDU na KUCO yapanga kufufua upya mgomo kaunti ya Mombasa

Muungano wa Madaktari KMPDU na ule wa Maafisa wa Kliniki KUCO kaunti ya Mombasa umetishia kususia kazi iwapo Serikali ya kaunti hii itashindwa kutekeleza mkataba wa maelewano waliotia saini pamoja na malipo ya mishahara na marupurupu ya wakati wa mgomo.

Wakiongozwa na viongozi wa kitaifa wa miungano hiyo wahudumu hao wa afya na madaktari walidai kuwa Serikali ya kaunti ya Mombasa ilikataa kuwalipa mishahara na marupurupu yao wakati walipokuwa wakishiriki mgomo miezi kadhaa iliyopita licha ya mahakama kutoa mwelekeo.

Waliongeza kwamba juhudi za kutafuta mwafaka kupitia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea ziligonga mwamba hali iliyoathiri utendakazi wao na utoaji huduma katika hospitali na baadhi ya vituo vya afya katika kaunti hiyo.

“Tukirejea watu watalipwa mishahara yao na watalipwa ile miezi yote ambayo hakuwa wakilipwa wakati walikuwa kwa mgomo.

Lakini mwezi mmoja umeweza ukaisha na tumeona yakwamba hii serikali kwetu imeweza kuandika barua na kusema ya kwamba watalipa tu kwa muda Fulani ambayo inaenda kinyume nay ale makubaliano ambayo tuliweza kuingia katika return to work agreement.

Madaktari wametutuma. Madaktari wamesema wapewe tu haki yao, haki ambayo imeandikwa katika ile return to work formula.”  Walisema maafisa hao.

Wakati uo huo Ismail Ramadhan Mwenyekiti wa Muungano wa maafisa wa Kliniki kaunti ya Mombasa, (KUCO) alidai kuwa maafisa kadhaa walirejeshwa kazini na kulipwa mishahara yao huku wengine wakisalia gizani.

Ni kauli iliyoungwa mkono na George Gibore Katibu wa muungano huo Kitaifa, ambaye alihoji kuwa mi kwa nini Gavana Nassir anakosa kuwalipa madaktari na wauguzi hao licha ya mahakama kumwagiza kufanya hivyo.

“La kustaajabisha gavana wetu wa Mombasa ni kama hafuati sheria manake kulingana na court oders zote ambazo zilizomfikia zinafaa turudi kazi na atulipe mishahara yote ambayo tulikuwa tunadai.

Kufikia sasa ni watu kadhaa ambao wanajulikana kwa maofisi ndio wamerudishwa kwa kazi, ni watu Fulani ambao wanajulikana kwa maofisi ambao wamelipwa mishahara,”  alidai Ismail.

Ikumbukwe kuwa muungano wa KMDU na KUCO ilisitisha mgomo wao uliodumu kwa kwa takriban miezi mitatu na zaidi baada ya makubaliano kuafikiwa ya kushghulikia matakwa yao.

BY NEWS DESK