Mahakama ya Upeo nchini imetoa maagizo na kusitisha kwa muda sehemu za uamuzi wa Mahakama ya Rufaa uliotangaza Sheria ya Fedha 2023, kuwa kinyume cha katiba.
Uamuzi huu umejiri kufuatia rufaa iliyowasilishwa na Waziri wa Hazina ya Kitaifa ya Fedha pamoja na maafisa wanne wa serikali dhidi ya uamuzi wa mahakama ya rufaa.
Katika maagizo hayo hayo yaliyoipa serikali afueni ya muda, mahakama hiyo ya upeo imesisitiza umuhimu wa kuimarisha utahbiti wa serikali na kuepuka hitilafu katika utawala wa umma.
Itakumbukwa kuwa Sheria ya fedha ya mwaka 2023 iliyopitishwa ilipata pigo kubwa mnamo Julai 31 mwaka huu pale Mahakama ya Rufaa ilipobatilisha kwa kile ilichotaja kuwa kinyume cha katiba kwa kutohusishwa wananchi.
Uamuzi wa mahakama ya rufaa ulikuwa umezua suitofahamu kuhusu hatima ya serikali kifedha na kuendeleza mipango yake hatua iliyopelekea serikali kutafuta mwafaka katika mahakama hiyo ya upeo.
By Mjomba Rashid