HabariNews

Mfanyabiashara Mashuhuri ‘Mombasa Cement’ Aaga Dunia

Mwanabiashara mashuhuri na mmiliki wa Kampuni ya Saruji ya Mombasa Cement Hasmukh ‘Hasuu’ Patel amefariki.

Kulingana na Msemaji wa familia Samir Bhalo, Patel ameaga dunia mwendo wa saa saba mchana wa leo alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali moja eneo la Nyali baada ya kuugua kwa siku mbili.

Patel Hassu maarufu kama ‘Mombasa Cement’ ambaye ndiye mmiliki wa kampuni hiyo ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 58.

Viongozi mbalimbali eneo la Pwani wametuma risala zao za rambirambi wakimtaja kama mwanabiashara aliyejitolea kikamilifu kuimarisha maisha na maslahi ya jamii kutokana na ukarimu wake.

Katika mtandao wake wa X Gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ameongoza ujumbe wa rambirambi wa serikali ya kaunti ya Mombasa na kumtaja kuwa mtu muhimu aliyekuwa karimu na aliyesimama kuunga mkono masuala ya jamii kaunti ya Mombasa.

Naye gavana wa Kilifi Gedion Mung’aro kwenye mtandao wake amemwmboleza Hasuu Patel na kumtaja rafiki wa kweli wa maendeleo aliyeheshimika katika jamii na ambaye daima alijali jamii zote pasi ubaguzi.

Kwa upande wake Waziri wa Madini na Uchumi wa baharini, Hassan Ali Joho amesema Mombasa na Pwani kwa jumla imempoteza kiongozi mkarimu aliyejitolea kuifanya Mombasa kuwa sehemu bora.

Ametaja baadhi ya kazi zake za kujtolea katika kuimarisha mazingira na hali za afya katika jamii, shughuli ambazo amesema zitaishi kukumbukwa.

Hasmukh ‘Hassu’ Patel aliyejulikana na wengi na kwa haraka kwa jina la Mombasa Cementkampuni ambayo anaimiliki hadi kufa kwake, atakumbukwa kwa miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa shilingi milioni 700 kubadilsha eneo la jaa la Kibarani kuwa bustani na kivutio cha wageni.

Kando na kulipia karo wanafunzi Hassu aidha aijitolea kuwalipia wagonjwa ada za hospitali.

By Mjomba Rashid