Walimu wanachama wa KUPPET kaunti ya Kwale wamefanya maandamano ya amani kuishinikiza tume ya kuajiri walimu (TSC) kutekeleza mkataba wa makubaliano yao kabla ya kurejea kazini.
Katibu wa chama hicho tawi la Kwale Leonard Oronje, ameongoza walimu hao katika maandamano na kuendelea kupuuzilia mbali agizo la mahakama la kusitisha mgomo wao bila ya serikali kutimiza matakwa yao.
“Tunataka CBA ilie iliyopitishwa iwekwe mezani na kwanza tuiangalie kama iko sawa, kisha zile pesa wanatukata za marupurupu ya matibabu saa hizi imekuwa medical scheme ya walimu iboreshwe zaidi.” Alisema.
Walimu hao aidha wamemtaka mwajiri wao,TSC kuwaajiri walimu wa JSS kwa mkataba wa kudumu mbali na kuwaongezea mishahara yao, huku wakipuuzilia mbali agizo la mahakama na kwamba hawatarejea madarasani.
“Agizo la mahakama kwani ni la walimu pekee na wengine hawafuati? Tungeomba Rais aanze yeye kuheshimu mkataba na sheria ya korti na walimu ndio tutafuata.” Alismea mmoja wa walimu hao.
Kando na hayo walimu hao wanashinikiza kupandishwa vyeo kwa walimu ambao wamehudumu kwa muda mrefu huku wakiwaonya wanasiasa dhidi ya kuingilia majukumu ya TSC.
“Hawa wabunge pia ndio saa hii wanaamua nani atakuwa Mwalimu mkuu wapi, nani atakuwa naibu wapi na mwalimu wapi atatakohamishwa, tafadhali wakome wasingize siasa waache kuingilia tume hutu kama TSC, na TSC iangalia CPG itolewe ama ibadilishwe na kufanyiwa marekebisho ile acting administrators waidhinishwe.” Walisema.
Wamewasuta walimu wakuu kwa kile walichodai kutumiwa na TSC kuwatishia walimu wakiwakata wakuu hao kukoma kuwatishia wanachama wao wanaoshiriki mgomo huo ili kutetea haki yao.
BY BINTIKHAMIS MOHAMMED