Muungano wa Majaji na Mahakimu nchini (KMJA) sasa umempa Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli makataa ya siku 14 kuomba msamaha kufuatia
kundolewa kwa walinzi jaji Lawrence Mugambi.
Masengeli ambaye mnamo Ijumaa wiki jana alihukumiwa kifungo cha miezi gerezani kwa kudharau mahakama ametakiwa kuwarejesha walinzi hao mara. Katika kikao na waandishi wa habari Rais wa Muungano huo Patrick Otieno amesema kuwa watamchukuliwa hatua za kisheria Inspekta wa polisi aliyewapigia walinzi hao na
kuwaondoa, hatua ambayo ameitaja kuhujumu utendakazi wa Idara ya mahakama na uhuru wake.
Naye Naibu Rais wa muungano huo, Rhoda Yator, ameeleza kuwa kitendo hicho kimeashiria kuwapa hofu majaji ambao wanaweza kupitia hatua sawia kwa kuendelea kushikilia haki na kusimamia sheria.
By Mjomba Rashid