Serikali ya kaunti ya Mombasa kupitia Wizara ya Utalii
imeweka wazi ratiba na mipango ya kaunti hiyo
itakayotumika kuadhimisha Siku ya Utalii Duniani
ambayo husherehekewa Septemba 27 kila mwaka
Akizungumza na Sauti ya Pwani Waziri wa Utalii, Utamaduni na
Biashara kaunti hiyo Mohammed Osman amesema kuwa
maandalizi ya kuadhimisha siku hiyo yangali yanaendelea huku
washikadau wote wakilenga kuwa na hafla ya kufana hapa
Mombasa.
Waziri huyo aidha ameweka wazi ratiba na sehemu mbali mbali
zitakazotumika kuandaa baadhi ya michezo na pia hafla muhimu
akisema sehemu hizo ni kivutio cha watalii na burudani hali
ambayo itanogesha maadhimisho ya siku hiyo ya utalii hapa
Mombasa.
“Kila mwaka Wiki ya Utalii Duniani ya Umoja wa Mataifa imekuwa
ikifanyika kuanzia tarehe 25 hadi 29, nak ama Mombasa
tutasherehekea kuanzia tarehe 26 mpaka 29, siku mabyao
Ulimwengu itaadhimisha Siku ya Utalii Duniani tumeandaa
mipango mingi sana, kuanzia tamaduni, vyakula na mashindano
mbalimbali ya kuvutia utalii na uwekezaji,” akasema.
Kauli ya waziri inajiri huku maadhimisho ya siku hiyo ya utalii
yakitarajiwa kuanza rasmi septemba 25 kilele chake kikiwa
Jumapili ya septemba 29 mwaka huu.
BY ISAIAH MUTHENGI