HabariNews

Gavana Nassir ajitenga na Madai ya Kutekwa nyara na Kulawitiwa Kwa Mwanablogu

Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharif Nassir amevunja kimya chake kuhusu madai ya kutekwa nyara na kulawitiwa kwa mwanablogu mmoja.

Na licha ya kubaini kukerwa mno kuhusishwa yeye na familia yake, Gavana Nassir amejitenga mbali na tuhuma za kuhusika na utekaji nyara na kulawitiwa kwa mwanablogu aliyemkashifu na kumtusi.

Akihutubia wanahabari Afisini mwake Gavana Nassir ameeleza kusikitishwa na shutma hizo akilitaja tukio kuwa la ‘kinyama’ na kwamba inashtusha kuwa yeye na mama yake wanahusishwa na kitendo hicho.

“Katika maisha yangu yote, mimi ama familia yangu yote hatujawahi kujibu wala kujibizana na yeyote wala kuhusiaka kwenye vurugu. Hata katika majukwaa ya kisiasa, sera yangu haijakuwa ya kumtaja yeyote kwa jina wala kuwatusi ama kutumia lugha chafui dhidi yao,” akasema Gavana.

Gavana Nassir aidha amesema hahusiki kamwe na masaibu yaliyomfika mwanablogu huyo huku akikana madai ya kukataa kuandikisha taarifa katika makao makuu ya upelelezi huku akidai kuwa baadhi ya viongozi wa kisiasa hasa mahasimu wake ndio wamepanga njama ya kumharibia jina.

Na kwa wale wenye kusema kuwa sina nia ya kuandika taarifa, hamna la ukweli. Niliitwa na tumeandikiwa tena kuwa hatutakikani (kuandikisha taarifa) kwa wale wenye kujaribu kuniumiza kisiasa, ukweli utakuja kudhihirika.”

Wakati uo huo Gavana huyo ameeleza kuhangaishwa kuhangaishwa kwa familia yake na baadhi ya maafisa wa kaunti hiyo, japo akieleza matumani ya ukweli wa kashfa hiyo kubainika.

Mamangu, mama wa miaka 74 anajulikana hata hataki usafiri wa magari wala usalama, hupanda tu tuktuk nashindwa kwa nini anahusishwa katika hili. Nasema wale wanaofanya hivi, leo wanaojaribu kwa sababu ya siasa kuniumiza mimi na kuiumiza familia yangu, ukweli utakuja kudhihiri.” Akasema Gavana Nassir.

Ikimbukwe kuwa mwanablogu huyo kwa jina Bruce John mwenye umri wa miaka 24 aliyeikashifu kaunti ya Mombasa n ahata kumtusi mamake gavana Nassir, anadaiwa kutekwa nyara nyumbani kwake Bamburi mnamo Septemba 12 na kundi la takribani maafisa 20 wa kaunti.

Kundi hilo liliripotiwa kumshambulia na kisha kumlawiti kabla ya kumtupa katika jaa la Mwakirunge alikookotwa na wasamaria wema.

Tayari washukiwa wanne kuhusiana na kesi hiyo wamekamatwa na kufikishwa mahakamani Shanzu walikokana mashtaka yanayowakabili, huku wakiendelea kuzuiliwa kwa siku 14 wakisubiri uchunguzi na hatma ya dhamana yao.

By Mjomba Rashid