HabariNews

Mahakama Kuu Yakataa Kusitisha Mchakato wa Bunge Kujadili Hoja ya Kumbandua Gachagua

Masaibu ya Naibu wa Rais Rigathi Gachagua yanazidi kuendelea, baada ya Mahakama Kuu kukataa kutoa maagizo ya kuzuia Bunge kushughulikia hoja ya kumbandua.

Kesi iliyowasilisilishwa mahakamani humo na aliyekuwa Katibu Mkuu wa UDA na Seneta Kakamega Cleopas Malala ilikuwa ikitaka kuzuia Mabunge ya Seneti na Kitaifa kuwasilisha, kujadili na hata kuifanyia kazi hoja yoyote ya kutaka kumbandua Gachagua.

Malala amesema kwamba mabunge hayo mawili yanakosa usawa wa kijinsia wa thuluthi mbili hivyo yako kinyume cha sheria.

Hakimu Bahati Mwamuye ameliagiza bunge la kitaifa kueleza majibu yao ifikapo Alhamisi Oktoba 3 mwaka huu sawia na Malala kuwasilisha hoja zake mahakamani Ijumaa endapo atahitajika.

Gachagua anakabiliwa na madai yakiwemo utumizi mbaya wa ofisi, ukiukaji wa kipengee cha 10 cha katiba kuhusu utawala, tuhuma za ukabila kwa kuendeleza siasa za eneo moja la Mlima Kenya na kutenga maeneo mengine na madai ya ufisadi kwa kujilimbikizia mali kwa kutumia fedha za mlipa ushuru kwa kununua hoteli za kifahari katika kaunti za Nyeri, Nairobi na Kilifi.

Kiongozi wa walio wengi bungeni Kimani Ichungw’ah amehakikisha kuwa mswaada huo utawasilishwa bungeni kesho Jumanne saa nane na nusu mchana.

Ikumbukwe kuwa ili mswada huo kuwasilisha utahitahitaji uungwaji mkono wa wabaunge 233, huku tayari ikisadikika kuwa wabunge 302 wametia saini kuunga mkono hoja hiyo kuwasilishwa.

Kesi hiyo ya kupinga kubanduliwa kwa Naibu rais itatajwa Oktoba 7.

By Mjomba Rashid