HabariKimataifaLifestyleNews

Makadinali wote Duniani Kukutana Vatican; Kipi Kitafuata Baada ya Kifo cha Papa Francis?

Makadinali wote Duniani Kukutana Vatican; Kipi Kitafuata Baada ya Kifo cha Papa Francis?

Kufuatia kifo cha Papa Francis, kilichotangazwa na Vatikani siku ya Jumatatu, Wakatoliki kote ulimwenguni wanakuwa katikati hali ya ati ati wakijaribu kutafakari ni nani atakayemrithi.

Kwa kuzingatia asili ya uteuzi wa kardinali Francis aliofanya wakati wa upapa wake, ni bayana kutakuwa na matarajio kwamba mrithi wa papa wa Argentina atakuwa mtu mwengine asiye mwenye asili ya kizungu kutoka Ulaya.

Inatajwa kwamba kama ilivyokuwa kwa Francis mrithi wa wadhfa huo mkuu na muhimu kwa wakatoliki duniani anaweza kuwa mtu mwingine wa maendeleo, kinyume na mrengo wa kihafidhina wa Kanisa hilo lililoko Vatican Italia.

Na mrithi wa Papa huchaguliwa na Makadinali ambao huwa ni washirika wa karibu wa papa, wanaoendesha idara muhimu katika Vatikani na dayosisi kote ulimwenguni.

Makadinali hao kutoka kote ulimwenguni kwanza hupanga tarehe ya kuanza kwa ‘Kongamano Kuu’ baada ya kuanza kuwasili Roma katika siku zijazo.

Makadinali hao aidha Wataamua tarehe ya mazishi, ambayo lazima ifanyike kati ya siku ya nne na ya sita baada ya kifo cha papa, na katika ushirika wa “novemdiales,” siku tisa za maombolezo.

Papa anapofariki au kujiuzulu, makadinali hao walio na umri wa chini ya miaka 80 wanastahili kuingia katika mkutano wa siri ili kuchagua kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki la Roma lenye takribani waumini bilioni 1.4 kutoka miongoni mwao.

Kura hiyo tata itafichua ikiwa makadinali wa sasa ambao wengi wao waliwekwa hapo na mwendazake papa Francis, iwapo wanaamini kukumbatia kwake maadili ya kijamii ya kiliberali na ajenda yake ya mageuzi ya kimaendeleo imekwenda mbali sana na ama iwapo muda wa kupunguzwa unahitajika.

Hadi kufikia sasa kulikuwa na jumla ya makadinali 252; na 135 kati yao ni makadinali wapiga kura chini ya 80. 109 kati ya wapiga kura waliteuliwa na papa Francis, 22 na mtangulizi wake papa Benedict na watano waliteuliwa na John Paul wa II.

Hata hivyo, mchakato wa uchaguzi utakaofanyika mara baada ya Francis kuzikwa ni wa siri sana na hakuna kitakachokuwa na uhakika hadi moshi mweupe ukitoka kwenye bomba la Sistine Chapel utakaoashiria ulimwengu kuwa papa mpya amechaguliwa.

Kwa sasa Kanisa Katoliki limeingia katika kipindi kinachojulikana kama “Sede Vacante” ambapo kardinali mkuu huchukua shughuli za kila siku hadi papa mpya atakapochaguliwa.

Kardinali, anayejulikana kama ‘camerlengo’ au (“chamberlain”), katika suala hili Kevin Farrell mwenye asili ya mataifa mawili ya Marekani na Ireland, aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo na Francis mnamo Februari 2019 ndiye afisa pekee wa ngazi ya juu katika uongozi wa Kanisa kusalia katika wadhifa huo, huku wengine wote wakihitajika kujiuzulu kufuatia kifo cha papa.

Jorge Mario Bergoglio raia wa Argentina maarufu Papa Francis ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 88.

Alikuwa papa wa kwanza asiye Mzungu (asyiye na asili ya Ulaya) katika kipindi cha karibu karne 13.

By Mjomba Rashid