HabariNews

Mlanguzi sugu wa Mihadarati akamatwa na Maafisa wa Kupambana na Mihadarati mjini Malindi

Maafisa wa upelelezi kutoka kitengo cha kupambana na Mihadarati mjini Malindi Kaunti ya Kilifi wamemnasa mshukiwa sugu wa ulanguzi wa dawa za kulevya aina ya heroin.

Salim Pater Katana amekamatwa na vifurushi 38 vya heroini zenye uzani wa kilo 3.635 na thamani ya shilingi milioni 14.5 katika soko.

Hii ni kufuatia taarifa za kijasusi zilizopelekea maafisa hao kufanya msako na kumnasa mafichoni kwake eneo la Ngerenya, alikopatikana amezificha kama hazina pamoja na shilingi 13,000 pesa zinazoaminika kuwa faida za biashara hiyo haramu.

Katana kwa sasa anaendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Malindi akisubiri kufikishwa Mahakamani.

By News Desk