HabariNews

Watahiniwa Zaidi ya 965,000 Waanza Mitihani ya Kitaifa KCSE

Mitihani ya Kitaifa kidato cha nne KCSE imeananza rasmi hivi leo huku wahiniwa 965,501 wakitarajiwa kufanya mitihani hiyo kote nchini.

Idadi ya waliosajiliwa kufanya mtihani mwaka huu imeongezeka kutoka watahiniwa 903,138 waliofanya mitihani hiyo mwaka uliopita.

Kundi la kwanza la watahiniwa hao wameanza mitihani yao ambapo wiki hii mitihani iliyoratibiwa kufanywa ni ya somo la Lugha ya Kifaransa, Kijerumani, Kiarabu, Lugha ya Ishara, Somo Music na Sayansi ya Nyumbani.

Mitihani hiyo inafanywa katika vituo 10,755 vilivyosajiliwa rasmi kote nchini.

Haya yanajiri huku viongozi wa chama cha walimu KNUT wakiitaka Serikali kuwahakikishia walimu na wanafunzi usalama wao hasa katika maeneo yanayokumbwa na mizozo.

By Mjomba Rashid