Ukosefu wa Vitambulisho vya Kitaifa kwa watahiniwa wa kibinafsi (private candidates) imetajwa kuwa changamoto kwa watahiniwa wa mwaka huu Kaunti ya Kwale.
Akizungumza baada ya kufungua kasha la mitihani eneo Bunge la Matuga Mkurugenzi wa elimu Kaunti hiyo Ahmed Abdi amesema haijabainika iwapo watahiniwa hao wa kibinafsi walichelewa kujisajili kupata vitambulisho hivyo au tu kutokuwa na ufahamu mwafaka kuhusu stakabadhi hitajika wakati wa kujisajili kwa mtihani huo wa kitaifa ikizingatiwa wana umri wa kati ya miaka 18 na 20.
“Shida ni kuwa huenda walichelewa kujisajili kupata ID ama hata hivyo hawakuenda kuzifuatilia kupata. Changamoto ni kuwa mambo ya ID na vijijini ni kizungumkuti maana wengi waliojisajili wanatokea kijijini ndio waje huku kufanya mtihani huenda mtu ni mkubwa lakini hajashughulika kutafuta, lakini wav yeti vya kuzaliwa na kuna mambo mengi tunayaangali kujua haswa kama ndiye mwanafunzi ama siye.” Akasema.
Vile vile Abdi amesema kuwa katika mtihani huu wa KCSE 2024 watahiniwa 69 wanafanya kama watahiniwa huru wa kibinafsi huku idadi kubwa ya watahiiwa hao ikitokea eneobunge la Kinango na Samburu kwa kuwa na watahiniwa 30.
Wakati uo huo Mkurugenzi ameliomba Baraza la mitihani KNEC kuanzia mwaka ujao kuwageuzia kituo cha kufanyia mtihani kwani wengi imewalazimu kuhama makwao na pia kukodi Sehemu ya muda ili kuweza kufanya mtihani wao badala ya kusafiri mwendo mrefu kwani wanaweza kufanya katika maeneo Bunge yao.
“Idadi ni kubwa na wengi wanatokea mbali kuja kufanya mtihani kwa kituo kimoja hiki (Kwale Seminary) na inajumusha wanafunzi 39 na kati ya hjawa 30 wanatoka Kinango na Samburu. Sasa idadi inasajili ni kubwa sana tumeandikia Baraza la kitaifa la Mitihani, KNEC ili tuwazuie wale watakaofanya miaka ijayo wafanyie huko waliko.”
Watahiniwa wa kibinafsi 25 wakiwa walijisajli eneo la Msambweni na 14 wakitoka Matuga wakifanyia mitihani hiyo katika shule ya upili ya Kwale st. Mary’s high school Seminary.
By Bintikhamis Kadide