HabariNews

Taasisi ya Masoroveya Nchini Kushirikiana na Wadau Kuwakabili Matapeli katika Sekta hiyo

Taasisi ya Masoroveya nchini, ISK imeapa kukabiliana na matapeli wanaojifanya kuwa masoroveya na kuwalaghai Wakenya.

Akizungumza na wanahabari hapa jijini Mombasa katika Kongamano la 9 la Kimataifa la Masoroveya mnamo Alhamisi Novemba 7, Rais wa Taasisi hiyo Erick Nyadimo alibaini kuwa suala hilo limekuwa kero na kuathiri pakubwa sekta ya ardhi nchini.

Nyadimo alisema ISK inashirikiana na washikadau mbalimbali wa sekta ya ardhi kulikabili suala hilo huku akiwahimiza wakenya kupiga ripoti kesi zozote za utapeli kutoka kwa masoroveya ambao walishindwa kutoa huduma walizoafikiana ili hatua mwafaka kuchukuliwa.

Tunafanya kazi pamoja na washikadau wote wa Bodi za usajili kuhakikisha kuwa tumewakabili vilivyo matapeli. Tunahimiza umma kutoa taarifa za ulaghai kwa taasisi zetu za ISK, kwa idara ya upepelelezi na makosa ya jinai  DCI ama tume ya madili na kupambana na ufisadi nchini EACC kuhusu visa vya wanakandarasi kukosa kutoa huduma jinsi inavyotakikana  kwa mujibu wa muktaba wa maafikiano ili hatua za haraka za kisheria zichukuliwe kukabili na kutatua  masuala hayo.” Alisema Nyadimo.

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi na mipangilio ya mji kaunti ya Mombasa Mohammed Hussein Mohammed alitoa hakikisho kwa Wawekezaji wa ardhi kuwa watalindwa dhidi ya matapeli ili kuepukana na mizozo ya masuala ya ardhi inayochipuza.

Waziri huyo alisema seriakali ya kaunti ya Mombasa inashirikiana na idara husika za ardhi sawia na kutekeleza sheria hitajika ili kulinda maskwota na wawekezaji dhidi ya hasara.

Masuala ya Ardhi na mashamba yana hisia kali na migororo  kila mahali haswa hapa mombasa.  Serikali ya kaunti ya mombasa inahakikisha  kuwa imepunguza migogoro hiyo kwa kushirikiana na wizara ya Ardhi na pia tume ya Ardhi  kwa kuweka sera na sheria kuwa maskwota wote wamepewa makazi na wawekazi wote wanaojihusisha na ununuzi wa mashamba hawajakadiria hasara. Jukumu letu kuu ni kuwapa maswota makazi na kuhakikisha wawekaji wa ununuzi wa mashamba hawakadirii hasara,” Alisema

Kongamano hilo la 9 la ISK linaandaliwa wakati visa vya unyakuzi wa mashamba vikisalia donda sugu nchini ambapo matapeli wanaojifanya kuwa masoroveya kwa muda wamekuwa  wakiwalaghai Wakenya.

BY ISAIAH MUTHENGI