Makala ya sita ya dimba la Rashid Abdhalla Supercup hatimaye yamewadia huku timu 32 zikitatarajiwa kuwania ubingwa wa mashindano hayo ya kipekee mwaka huu.
Mashindano hayo yatachukua muundo mpya utakaojumuisha timu 32 ,16 kutoka Kaunti ya Mombsa na 16 kutoka Kaunti ya Kwale amabzo zimepangwa kwenye makundi manne mtawalia, kila kundi likiwa na timu nne.
Hii ni kufuatia droo iliyoandaliwa Jumatatau Mei 12 katika shule ya akademia ya Aghakhan mjini Mombasa ambayo iliweka bayana makundi yote.
Akizungmza baada ya kukamiika kwa droo hiyo mwandalizi wa mashindano hayo Rashid Abdhalla alisisitiza azma ya kukuza vipaji katika ukanda wa pwani.
Abdalla amesema hatua ya kujumuisha timu kutoka kaunti hizo mbili n njia ya kutoa fursa sawia kwa timu kushiriki dimba hilo na kuhimiza umoja na ushindani kupitia soka.
“Nina imani kwamba mwaka huu tutaona vijana wengi wakipata fursa za kucheza mpira na kukuza vipaji vyao.
Kutakuwa na mawakala ambao watakuwepo kuwatizama vijana wetu kutoka haopa nchini na wengine kutoka mataiofa ya nje ili wachezaji wapate nafasi pia ya kucheza sit u katika timu kubwa za hapa nchini bali pia vilabu kutoka nje.” alisem Abdalla
Rashid hata hivyo ametoa wito kwa timu zote zitakazoshiriki kudumisha nidhamu kwenye mashindano hayo ili kuwavutia wawekezaji zaidi.
“Nidhamu ndio kitu cha msingi na ikiwepo ndio amabapo wawekezaji watapata urahisi wa kuwekeza fedha zao.’” Abdallah alionya.
Kwa upande wake kocha wa zamani wa harambee stars Ghost Mulei amepongeza juhudi za kukuza vipaji kupitia mashindano hayo akisema yametengeneza njia kwa wachezaji wachanga kuonyesha vipaji.
Mulei ametambua eneo la pwani kama kitovu cha vipaji hasa katika ulingo wa soka na kuahidi kufanya kazi kwa ukaribu na wandalizi wa mashindano hayo kuhakikisha vipaji vinatambulika katika soka ya chini na hata kimataifa.
“ Tutafanya kazi na Rashid Abdalla wakati wa toleo hili ili kusaidia kutambua na kukuza vipaji bora. Coast ina baadhi ya wachezaji bora nchini, na wanastahili jukwaa la kung’ara,” alisema Mulei.
Makala ya sita ya kitufe hicho yanayatrarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na mihemko ya aina yake na kutoa juwaa la kipekee kwa vijana kuendelea kukuza vipaji vyao.
MAKUNDI
Kwale
Kundi A
Denmark
Kundutsi
Green boys Mshale fc
Kundi B
Dumna
Generation United
Kinango Raptors
Nasty milan
Kundi C
Lazium
Fafada
Similani
Makamini combine
Kundi D
Azam Utd
Vivah Manyotta
Blue Rangers
Vanga Utd
Mombasa
Kundi A
Congo Boys
Shanzu Utd
Kishada Soccer
Wananyuki Fc
Kundi B
BandariYouth
Shimanzi Fc
Fayaz Bakers
Vimbwanga
Kundi C
Mombasa All Stars
Tononoka combine
Ziwani fc
Change Youth Academy
Kundi D
Paranja biro
Mvita young stars
Kiembeni rebels
Sparki youth
By Mohammed Mwajuba.