Wanaharakati mbalimbali wa kutetea haki za kibinadamu wamependekeza kubuniwa kwa mbinu mbadala za kuzuia mauaji ya kikatili dhidi ya wanawake na wasichana pamoja na kukomesha visa vya dhulma za kijinsia.
Wakiongozwa na Yusra Mohammed Kinango kutoka kwa shirikisho la wanasheria wananwake Kenya (FIDA) alipendekeza kuwekwa kwa mbinu ya kidigitali ya kuripoti na kurekodi visa vya kutishiwa maisha kwa wanawake akiitaja mbinu hiyo itakayopunguza mauaji ya kiholela kwa kuwa washukiwa wataogopa kufuatiliwa lutokana kutambuika kwa njama yake.
“Njia ya kwanza kumaliza visa hivi kwa mfano ni kuzuia mauaji ya wanawake ni kuwekwa kwa mfumo wa majibu, A RESPONSE SYSTEM ili hawa watu wanapotishiwa wanakuja kuripoti na kupitia kwa njia hii mapema kutakuwa na ufuatiliaji kwa hiyo mhalifu akijua amegundulika ataghairi nia yake ya kutekeleza mauaji.” Alisema Bi. Kinango
Hata hivyo Bi. Kinango aliongeza kuwa ni vyema zaidi iwapo serikali itabuni namba huru za kupiga simu ili kuripoti visa vya dhulma za kijinsia na ukatili hususani mtuakiwa kwenye hatari zaidi.
“ni vyema zaidi iwapo kutakuwa na namba za kupiga simu kwa kuwa mtu awapo kwenye hatari mara nyingi huwa vigumu kuripoti, na kwa kuwa kesi za dhulma za kijinsia huchukua mda mrefu mahakamani upata haki kutokana na mhalifu kuwa na haki hili huenda likapunguza mda wa kushughulikiwa kwa kesi hizo kutokana na kwamba kutakuwa na ushahidi wa kutosha.”
Kwa upande wake Mariam Baya, Afisa mkuu wa kushughulikia ukatili wa kijinsia katika shirika la YWCA alithibitisha kwamba kufikia mwezi huu kama shirika lilipokea kesi 700 za dhulma za kijinsia kote nchini.
Baya alidokeza kuwa kuna mwanya mkubwa katika kutoa takwimu kamili za visa vya ukatili wa kjinsia.
“Tunatambua kwamba serikali imejitahidi kukabiliana na visa hivyo lakini nataka jamii itambue kwamba bado kuna mwanya mkubwa katika kuripoti visa vya ukatili pamoja na habari potofu katika jamii na tunaimani kwamba kupitia kwa vikao vua utoaji maoni ya visa vya dhulma za kijinsia wakenya watapata haki pamoja na mahali salama kuishi kwa waathiriwa hususani kaunti hii ya Mombasa ikizingatiwa kwamba kufikia saa hata mahakama iliyotengewa kesi hizi ilifungwa.” Alidokeza Baya
Ikimbukwe kwamba jopokazi maalum lililoteuliwa na rais william Ruto likiongozwa na aliyekuwa Naibu Jaji mkuu Nancy Barasa lilibaini kuwa visa 700 vya ukatili na mauaji ya wanawake viliripotiwa kote nchini tangu mwaka 2016.
BY NEWS DESK