Rais William Ruto ameelezea kusikitishwa kwake na kukwama kwa mradi uboreshaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kutokana na kufutiliwa mbali kwa mkataba wa Adani Group.
Akielekeza hasira zake kwa Wakenya waliopinga mradi huo rais aliwasuta na kupuuzilia mbali juhudi za waliopambana kusitisha shughuli za ukarabati wa uwanja huo kupitia kampuni ya kimataifa ya Adani.
Akizungumza wakati wa hafla kuweka jiwe la msingi kwa Mradi wa Utengenezaji Chuma wa Devki katika Kaunti ya Taita Taveta, Rais Ruto alikasirishwa na Wakenya kupinga mpango huo ambao ungemfanya Adani kutoa shilingi 260 kuboresha uwanja wa ndege kupitia muundo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).
Kiongozi huyo wa taifa alibainisha kuwa Wakenya kama hao hawana njia mbadala ya kuboresha uwanja wa ndege lakini kila mara wanarushiana matusi na kupinga sera za utawala wake.
“Niliona hata watu wengine wanaglorify ati Airport imesimamishwa sasa wale wamesimamisha ujenzi wa airport ni mashujaa, mashujaa wa kitu gani? Airport pale iko kwa runaway, airport inavuja iko kwa tent nchi zingine wanejenha airport, yetu hapa kenya sijui ni ya aina gani watu hapa wanasema eti tumeshinda kusimamiamisha airport. What gain do you get?”
Aliwataja kuwa wasiopenda maendeleo kwani uwanja huo u katika hali mbaya mno na ulihitajia uwekezaji ili kukarabatiwa.
“Unapata faida gani unaposimamisha ujenzi wa uwanja wa ndege katika nchi yako? Hujui jinsi utakavyojengwa, wale wanapinga, ata hawajai kanyaga, unapinga tu.”
Rais alisisitiza tena kwamba utawala wake bado utaanza kuboresha uwanja wa ndege ili kuinua katika viwango vya kimataifa, akitaja kuwa ana imani kuwa Adani Group ingefanya kazi bora.
By Mjomba Rashid