HabariNewsSiasa

Afueni kwa Gavana Mwangaza Mahakama Ikiongeza Muda wa Agizo la Kuzuia Kubanduliwa afisini

Gavana wa Meru Kawira Mwangaza amepata afueni baada ya Mahakama Kuu kuongeza muda wa agizo la kuzuia utekelezaji wa uamuzi wa Seneti wa kumtimua afisini kwa siku 120.

Jaji wa Mahakama Kuu Bahati Mwamuye mnamo Jumatano aliamua kwamba maombi ya Mwangaza yamekidhi kizingiti kinachohitajika ili kuongezwa kwa amri hizo.

Mahakama pia ilibainisha kuwa maslahi ya umma yanakubali kurefushwa kwa muda wa amri hizo, na kuongeza kuwa iwapo amri hizo hazitaongezwa basi kesi hiyo itakuwa mbaya ikiwa Mwangaza atashinda kesi hiyo.

Mahakama iliambiwa kuwa Mwangaza atapata madhara na kesi hiyo itakuwa zoezi la kinadharia tu.

Hii ina maana kwamba kesi hiyo itasikilizwa kikamilifu.

Akizungumza na wanahabari mnamo Jumatano baada ya uamuzi huo Gavana Mwangaza aliwashukuru wafuasi wake kwa kuendelea kumuunga mkono, akieleza matumaini ya kushinda kesi hiyo.

Nataka kuwashukuru nyote hasa wafuasi wangu kwa kuniunga mkono na naamini siku tulizopewa tutatii maagizo ya mahakama na naamini kile Mungu amempa mtu hakuna yeyote yule anaweza kukichukua.

Nina imani hizo siku zaidi ya 100 Mungu atafanya miujiza yake na hiyo ni imani yangu, naamini maombi ya wafuasi wangu hasa akina mama wa Meru walioniombea wamejibiwa.” Alisema.

Kesi hiyo itatajwa Desemba 20.

BY MJOMBA RASHID