HabariLifestyleNews

Rais Ruto awataka Wakenya kusherehekea kwa Kipimo na Uwajibikaji

Tusherekee sikukuu ya Krismasi kwa kiasi na kujizuia ili tudumishe utulivu.

Ni ujumbe wake rais William Ruto kwa wakenya na waumini wa dini ya kikristo nchini huku shamra shamra za krismasi zikizidi kunoga kote nchini na ulimwenguni.

Rais Ruto akiongoza taifa la Kenya kwa sikukuu hiyo amewataka Wakenya kusherehekea kwa kiasi na uwajibikaji.

“Tujue kwamba Krisimasi ni wakati wa sherehe na furaha, lakini pia tufanye yote tunayofanya kwa kiasi.”

Akizungumza katika ibada ya Krismasi Kanisani AIC Olipisiai kaunti ya Narok Rais Ruto pia aliwahimiza wazazi kuwaelekeza wanao kimaadili ili kuzuia uhalifu.

Tuwachunge watoto wetu tuwazuie na mambo ya madawa, mambo ya pombe na mambo ya tabia zisizo nzuri, pia tulinde familia zetu tujue familia ndio msingi wa taifa.” Alisema.

Wakati uo huo Kiongozi huyo wa taifa amewataka Wakenya kuzingatia nidhamu na kutumia raslimali za nchi vyema kuliendeleza taifa kiuchumi.

Ni wajibu kwetu, tuwe watu wenye nidhamu na kutumia raslimali Mungu ametupatia kwa njia nzuri, tuweze kuzalisha chakula, tuweze kuzalisha mazao inayotupatia pesa ndio tuweze kukuza uchumi wetu.”

By Mjomba Rashid