AfyaHabari

Chanjo ya Fizer Bio/tech yabainika kuzuia maambukizi ya corona kwa kiwango kikubwa

Chanjo dhidi ya virusi vya corona ya kampuni ya Fizer Bio/tech imebainika kuzuia maambukizi ya corona kwa kiwango kikubwa.

Chanjo hiyo ina uwezo wa kuzuia maambukizi kwa asilimia 94 kwa watu wa umri wowote, hali inayotoa matumaini ya kukabiliwa kwa janga la corona duniani ikiwemo kuchangia kuondolewa kwa masharti makali ya kuzuia maambukizi mfano agizo la kutokuwa nje, kuzuiwa kutosafiri, kutokaribiana na mengineo.

Kulingana na utafiti uliofanywa nchini Israel unaonyesha kwamba, miezi miwili baada ya baadhi ya raia wake kupewa chanjo ya fizer bio/tech dalili kali za corona zimepungua kwa asilimia 94, huku dalili miongoni mwa wagonjwa waliokuwa wamedhoofika kiafya zikipungua kwa kiwango hicho hicho.

Watu takriban milioni 1.2 walifanyiwa utafiti.

Haya yanajiri huku taifa la Ghana likiwa taifa la kwanza Afrika kupewa chanjo ya Astrazeneca huku Kenya ikitarajiwa kupata chanjo hiyo mwishoni mwa mwezi huu ambapo wizara ya afya ilisema dozi milioni 24 zitaletwa humu nchini.