HabariMombasa

Muungano wa wahudumu wa mabasi, matatu, tuk tuk na Boda boda wanaitaka serikali kulegeza masharti yaliyowekwa ya kuthibiti maambukizi ya virusi vya covid-19.

wanasema biashara zao zimedidimia kutokana na hatua ya kupigwa marufuku safari nyakati za usiku.

Wakihutubia waandishi wa habari katika ofisi za shirika la  kutetetea haki za kibinadamu la haki Afrika Mombasa, wanasema kunafaa kuwepo usawa kati ya wahudumu wa safari za ndenge pamoja na zile za reli ya kisa ambazo zinaendeshwa nyakati za usiku.

Wakati huo huo muungano huo umetoa makataa ya saa 24 kwa serikali kutoa majibu vyenginevyo wataandaa maandamano kushinikiza serikali kuondoa marufuku hio.

 

Na Nick Waita