HabariSiasa

Mjadala kuhusu kigezo cha mgombea nafasi ya uwakilishi wadi ….

Mkereketwa wa maswala ya Siasa mjini Mombasa Omar Abdhallah anasema wadhfa huo umevutia viongozi wengi sehemu za mashinani japo kigezo cha shahada huenda kikawa changamoto kwao.

Katika mahojiano ya Kipekee na Sauti ya Pwani Fm, Abdhalla amesema iwapo kipengee hicho kuhusu sheria ya uchaguzi hakitafanyiwa mabadiliko huenda kuwa na viongozi wenye shahada japo hawana tajriba ya uongozi.

Amesema kwa sasa viongozi wanaangazia sana swala la BBI na huenda seria hiyo ikakosa msukumo wa kufanyiwa marekebisho, hatua ambayo huenda ikawa na athari kwa mwananchi wa kawaida mashinani.

Kwa upande wake John Thuva Dzimba mwanaharakati wa siasa na mwenye azama ya kuwania wadi ya Kadzandani eneo bunge la Nyali, anasema kigezo hilo kinaathari kubwa kwa viongozi wengi hasa sehemu za mashinani.

 

Na Joseph Jira