AfyaFoodHabariLifestyleMakalaMombasa

Wakaazi wa Bofu Likoni Mombasa walalamikia ukosefu wa maji…….

Wakazi wa kata ndogo ya Bofu eneo bunge la likoni kaunti ya Mombasa wanalalamikia ukosefu wa maji wakisema kwamba kuna bwenyenye anayeshirikiana na viongozi katika kusambaratisha utoaji huduma ya maji eneo hilo.

Elija ochieng mkaazi wa eneo hilo anasema kwamba kero la maji limekuwa gumzo katika eneo hilo kwa muda mrefu kiasi cha kuwa wenyeji wa eneo hilo wameachawa katika hali  tata ya kutafuta maji  inhali wanalipa ushuru kama wakenya wa kawaida ,

Ochieng anasema kwamba kuna bwenyenye anayeshirikiana na baadhi ya viongozi katia eneo hilo kusamabaza maji kunyume na sheria na hata kuchangia kuchanganya maji ya chumvi na maji  safi ya mfereji.

Kadhalaka wenyeji hao wameshutumu vikali  mwakilishi wadi wa eneo hilo la Bofu wakisema kuwa kiongozi  huyo ni mwenye ubinafsi na ni mbaguaji katika utoaji  huduma kwa wakazi wa eneo hilo.