HabariKimataifaMakala

KWAHERI MAGUFULI.

Mwendazake  rais  wa tano wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Joseph Pombe Magufuli alizaliwa mnamo 29 October 1959 katika wilaya ya Chatu nchini Tanzania.

Alijiunga na Siasa ambapo aliongoza wizara mbali mbali na kugombania Urais kwa awamu ya kwanza Mwaka wa 2015, uchaguzi uliokuwa na ushindani kutoka kwa Edward Lowasa.

Magufuli alishinda uchaguzi huo na kuapishwa kama wa rais tano wa jamuhuri  hiyo  mnamo  5 novemba mwaka 2015

Katika muhula wake kwanza kama rais wa taifa  hilo, Magufuli alionekana   kama  kiungo muhimu katika kubadilisha maisha ya wananchi wake kutokana na msimamo dhabiti katika kupambana na ufisadi, ,uongozi, ubadhirifu wa fedha, unyanyasaji wa wanyonge miongoni mwa dhulma nyinginezo

Alifahamika sana kwenye mitandao kama rais wa kwanza kuenda kinyume na viongozi ulimwenguni baada ya janga la korona kubisha hodi.

Magufuli aliagiza raia wa jamuhuri ya Tanzania kutanguliza maombi katika harakati  za kukabilina na maambukizi ya virusi korona

Magufuli alinukuliwa akipinga vikali chanjo ya virusi vya korona akisema kuwa ingawaje maradhi mengine kama vile virusi vya ukimwi, saratani hadi kufikia corona bado hakujapatikanana dawa wala chanjo

Kutokana na masimamo wake mkali mwendazake  wakati mmoja alikinzana na uongozi wa taifa jirani la kenya baada ya kuchoma vifaranga vilivyotarajiwa kuingia nchini Tanzania kinyume na sheria ya taifa hilo.

Rais huyo wa tano ni msomi wa taluma ya elimu alikopata shahada ya kwanza ya kemia na hisabati katika chuo kikuu cha Dar es Salaam mnamo 1988 na badae kuendeleza masomo yake.

Alichaguliwa kama mbunge wa Chatu katika mwaka 1995 na hata kuhudumu kama naibu waziri katika wizara ya wafanyikazi, na kuwa waziri wa uchukuzi, ujenzi, kabla ya kuwania kiti cha urais mwakaka 2015 katika chama cha Chama cha mapinduzi na kuwania tena urais 2020 na kuibuka ushindi .

Mwendazake ameacha nyuma mke Janeth Magufuli.

Na David Otieno.