Habari

Magoha apuzilia mbali madai kwamba mtihani wa KCSE umeibwa……

Waziri wa elimu proffesa George Magoha anasema wizara yake haitalegeza kamba katika kuhakikisha kwamba kuna uadilifu katika mitihani ya kitaifa humu nchini.

Akizungumza huko Kisii aliposimamia zoezi la kufunguliwa kwa mitihani ya kcse mapema leo, Magoha anasema bado wanazifuatilia shule kadhaa kutoka Kisii, Isebania, Homabay na Migori kuhusiana na visa vya udanganyifu kwenye mitihani hiyo.

Aidha amehakikisha kwamba mtihani wa KCSE kamwe haujaibiwa kama inavyodaiwa.

 Wakati huo huo amewaonya wasimamiza wa mitihani hiyo kutochelewa kufika kwenye vituo vya mtihani.

Zaidi ya watahiniwa elfu 750 wanafanya mtihani wa KCSE mwaka huu.