Baadhi ya wakaazi katika kaunti ya Tanariver wamelalamikia uhaba wa wahudumu wa afya na vilevile vifaa vya kimatibabu katika hospitali ya Ngao sub county hali hii ikiwa imechangia utoaji wa huduma duni kwa wagonjwa wanaofika kutibiwa.
Wakiongozwa na Abdi Semi wamesema kwamba wahudumu wa afya wamelazimika kufanya kazi kwa zamu mchana na usiku pamoja na kuwa hitaji za huduma za ambulensi wametakiwa kulipa ada ya sh 6000 na 8000.
Aidha wamesema kuwa uhaba wa vifaa vya matibabu unashuhudiwa kwenye chumba cha kina mama cha kujifungua vilevile na chumba cha wagonjwa mahututi.
Wagle Abdi ambaye ni afisa wa shirika la kutetea haki za binadamu la Muhuri tawi la TanaRiver amesema kwamba wataishtaki seriakli ya kaunti hiyo iwapo hatua za haraka za kuimarisha mazingira ya kikazi hazirachukuliwa