Wazee wa Kaya chini ya muungano wa kitamaduni wa MADCA mjini Malindi sasa wanawataka viongozi wa kisiasa eneo hilo kuingilia kati ili kuzuia mauwaji ya kiholela ya wazee kwa tuhuma za uchawi.
Kulingana na mwenyekiti wa wazee hao Emmanuel Munyaya, viongozi wengi wa kisiasa wameiachia idara ya usalama pekee jukumu la kuwalinda wazee hao.
Munyaya amesisitiza haja ya viongozi kukomesha tabia hiyo, akisema kuwa baadhi ya wazee wanaopata hifadhi katika kambi za wazee ni jamaa wa karibu wa viongozi mashuhuri kaunti hiyo.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa masuala ya usalama mjini Malindi ustadhi Athman Ali Said amesema kuna haja ya jamii kuhamasishwa kuhusu umuhimu wa wazee.
Said anasema viongozi wamekuwa wakishirikiana na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ili kukomesha tabia ya mauaji ya wazee.