BurudaniHabari

Sekta ya Sanaa mjini Malindi yapigwa jeki…

Sekta ya sanaa mjini Malindi imepigwa jeki baada ya mwekezaji mmoja raia wa Italia kuanzisha mpango wa kuwasaidia wasanii wa kitamaduni eneo hilo msimu huu wa janga la Corona.

Mwekezaji huyo kwa jina Franco Cozi amesema mpango huo unalenga kuimarisha uchumi wa wasanii hao kwa kuwatafutia sehemu watakazotoa burudani kwa watalii mjini Malindi hasa katika mikahawa kwa kutumia ala zao za mziki wa kitamaduni.

Mmoja wa wasanii watakaonufaika na mpango huo ni Katoi wa Tabaka ambaye licha ya kupongeza juhudi hizo ametoa wito kwa serikali kuangalia maslahi ya wasanii Nchini ambao wengi wameshindwa kujikimu.

Ni kauli ambayo imeungwa mkono na mwenzake Kaingu Supi ambaye anaitaka serikali kulegeza baadhi ya masharti yake ili kupiga jeki sekta hiyo.

Mwekezaji huyo analenga kuwatafutia soko la ulaya wasanii hao huku wasanii kumi tayari wakiwa wamejiandikisha katika mpango huo.

By Joseph Yeri