Wizara ya maji na unyunyizaji mashamba pamoja na shirika la kitaifa la Kenya water for health organization, limeandaa kongamano la wadau kutoka kaunti 47 nchini kwenye kaunti ya Mombasa.
Kongamano hili linanuia kujadili kubuniwa kwa sera ya kitaifa ya usafi, uhifadhi wa maji taka pamoja na kuwepo kwa maji ya kutosha katika maeneo husika.
Kulingana na Richard Cheruiyot afisa kutoka bodi ya maji ni kuwa takriban wakenya milioni 6 ambayo ni sawa na asilia 12 wanaishi katika mazingira yasiyosafi hivyo basi sera hii itasaidia katika kulainisha usimamizi wa usafi wa mazingira.
By Joyce Kelly