Kenya imepokea mkopo wa shilingi bilioni 80.9 kutoka Benki ya Dunia ili kuisaidia katika bajeti yake na vilevile kukuza uchumi wa Afrika Mashariki ambao umezoroteka pakubwa kutokana na athari za janga la Corona.
Serikali ya Kenya imekuwa ikishinikiza sana kupata usaidizi wa kifedha kutoka nje ili kujaza upungufu uliopo katika bajeti yake kabla ya mwaka wake wa fedha kufungwa mwishoni mwa mwezi huu.
Utoaji wa mkopo ni sehemu ya Uendeshaji wa Sera ya Maendeleo ya Benki ya Dunia (DPO), ambayo inatoa fedha kwa msaada wa bajeti badala ya kufadhili miradi maalum.
Benki hiyo imesema baadhi ya fedha zitakwenda kuanzisha mfumo wa ununuzi wa bidhaa za kielektroniki ili kuboresha na kuweka wazi huduma za serikali.
By Joyce Mwendwa