Mbunge wa Eastleigh Yusuf Haji na mwenyekiti wa jamii ya wafanyabiashara mtaani humo Abdullahi Ahmed wamewaongoza wananchi na wafanyabiashara kuishinikiza serikali kuimarisha usalama katika eneo hilo.
Yusuf Haji amesema kuwa ameshirikiana na serikali ya kitaifa kuhakikisha wameekeza zaidi katika maswala ya usalama kwa kuwaajiri maafisa wapya.
Wakati huo huo Abdullahi Ahmed amesema watashirikiana na asasi za usalama kuhakikisha kuwa uhalifu ambao umekithiri mtaani Eastleigh umemalizika na kwa wakati huo akaishukuru idara ya usalama kutokana na juhudi zake .
Haya yanajiri siku chache baada ya wahalifu waliomteka nyara Hafsa Mohammed kukamatwa katika eneo la Kinangop.
By Allan Preston