Kuna uwezekano mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC Wafula Chebukati akaondolewa madarakani kabla uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022 kufika.
Kulingana na mchanganuzi wa maswala ya kisiasa wakili George Kithi, kufutiliwa mbali kwa matokeo ya kura za Urais mwaka 2017 kulitia doa utendakazi wa Chebukati hivyo itakuwa vigumu kwa wawaniaji wa kiti cha Urais kumuamini.
Kithi ambaye analenga kugombania Usenati kaunti ya Kilifi anasema Chebukati kwa sasa hana baraka za kisiasa hasa baada ya upinzani uliopinga matokeo ya 2017 kuungana na serikali.
Kauli ya Kithi inakuja wakati wabunge wa chama cha ODM wakitaka mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kutoidhini utoaji zabuni ya kuchapisha karatasi za uchaguzi mkuu ujao hadi tume hiyo ya uchaguzi ipate makamishna wapya.
By Reporter