HabariNews

Baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Kilifi sasa wanaitaka IPOA kuanzisha uchunguzi…

Baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Kilifi sasa wanaitaka mamlaka huru ya kuchunguza utendakazi wa polisi nchini IPOA kuanzisha uchunguzi dhidi ya polisi waliohusika katika ubomoaji wa nyumba za wakaazi wa kijiji cha Nayeni wadi ya Sokoni katika eneo bunge la Kilifi Kaskazini.

Kulingana na mwanaharakati wa kutetea maslahi ya jamii kaunti hiyo Stembo Kaviha  maafisa wa polisi walikiuka sheria na kuwavamia  wakaazi wakati wa usiku na kuwahangaisha kwa kuwavunjia makaazi yao.

Aidha Kaviha amewalaumu vikali viongozi wa kaunti ya Kilifi kwa kulifanyia siasa swala la ardhi akisema  kuwa suluhu la mizozo hiyo ni katika bunge la kitaifa.

Aidha mwanaharakarakati huyo ameishtumu vikali tukio hilo akisema kuna haja kwa wananchi kaunti hiyo kuelimishwa kuhusu haki zao za ardhi pia ameitaka tume ya kitaifa ya ardhi nchini NLC kuingilia kati swala hilo na kuhakikisha wakaazi wanapata haki yao.

BY NEWS DESK