HabariNews

MWENYEKITI WA TAASISI YA BARAZA LA WAHASIBU NCHINI GEORGE MOKUA APINGA KAULI YA WAZIRI MATIANG’I KUWA WAHASIBU HUHUSIKA NA KASHFA ZA UFISADI.

Mwenyekiti wa taasisi ya baraza la wahasibu nchini George Mokua amejitenga na kauli ya waziri wa maswala ya ndani ya nchi Dkt Fred Matiang’i kuwa wahasibu mara nyingi wanahusika katika kashfa za ufisadi akitoa mfano wa wahasibu 18 ambao wanachnguzwa na maafisa EACC.
Mokua akizungumza na vyombo vya habari amesema kuwa wahasibu nchini wana mchango mdogo katika ufisadi kwani wanafasi ya mwisho kabisa ikingatiwa kanuni za ununuzi na hata utoaji kandarasi, huku akisisitiza kuwa vita dhidi ya ufiasadi vinafaa kupiganiwa kwa ushairikiano wala sio kuonyeshea vidole vya lawama wahasibu nchini.
Aidha ametaja kuwa kuna wahasibu Bandia ambao wanapaswa kuondolewa ili kuhakaikisha kuwa vita vya ufisadi vinapiganwa kikamilifu.