HabariMazingiraNews

NEMA YATAKA WAEKEZAJI BINAFSI WA TIMBO ZA MAWE NA MCHANGA KUREKEBISHA SEHEMU YALIYOFANYIWA UCHIMBAJI BAADA YA KUMALIZA KAZI.

Halmashauri ya mazingira nchini NEMA imewataka waekezaji binafsi wa timbo za mawe na mchanga kuhakikisha sehemu zinafanyiwa uchimbaji zinarekebishwa baada ya kukamilisha shughuli zao ili kuwaepusha wenyeji na majanga.
Mkurugenzi wa NEMA Kwale Godfrey Wafula ameyataja maeneo ya Tiwi, Waa na Mwache kuwa na mashimo makubwa yaliyotokana na ukataji mawe akihofia huenda yakahatarisha maisha ya wakaazi endapo yatajaa maji msimu huu wa mvua.
Wakati uohuo amewaonya waekezaji hao dhidi ya kuendeleza shughuli hizo karibu na maeneo ya makaazi.

>> News Desk.