HabariMazingira

Wadau katika sekta ya mazingira sasa wanaitaka serikali kuweka mikakati thabiti.

Wadau katika sekta ya mazingira sasa wanaitaka serikali ya pamoja na zile za mataifa jirani kuweka mikakati thabiti ili kuhakikisha mipira ya plastiki haitumiki tena. Wakizungumza kwenye zoezi la kusafisha ufuo wa bahari hindi mjini Malindi kaunti ya Kilifi, wadau hao wameitaka serikali kuzingatia uhifadhi wa mazingira kikamilifu.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa idara ya mazingira kaunti ya Kilifi Zainab Mohamed, asilimia kubwa ya uchafu baharini husababishwa na plastiki hata baada ya serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.
Aidha wamezitaka nchi za kigeni kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa mazingira hasa ya baharini yanatunzwa wakidai uchafu mwingi baharini hutoka katika nchi hizo.

>> News Desk…