Tume ya uchaguz na mipaka nchini IEBC inatarajiwa kuanza shughuli ya uchapishaji karatasi za kura huku karatasi za Useneta, ubunge na uwakilishi wa kike na wadi zikitarajiwa kuwa za kwanza kuchapishwa.
Hatua hii inajiri baada ya Mahakama kuu kutupilia mbali kesi iliyokuwa imewasilishwa na mgombea urais wa Chama cha Safina Jimmy Wanjigi akitaka jina lake lijumuishwe.
Akitoa uamuzi huo jaji Jairus Ngaa alisema wanjigi hakutoa Ushahidi wa kutosha kuthibitisha kwamba shughuli ya kuchapisha karatasi hiz inastahili kusitishwa.
Wanjigi aliwasilisha kesi mahakamani baada ya tume ya IEBC kukataa kumuidhinisha kuwania urais kwa kukosa digrii.
Hapo jana mahakama Kuu iliagiza IEBC kuhakikisha picha za wagombea wenza wa urais na ugavana zinajumuishwa katika karatasi za kupigia kura.
>> Editorial Desk…