HabariNews

wakazi ukanda wa pwani, wameshauriwa kuepuka mila na tamaduni zinazowakandamiza wanawake na watoto wa kike.

wakazi ukanda wa pwani, wameshauriwa kuepuka mila na tamaduni zinazowakandamiza wanawake na watoto wa kike.

Kulingana na rais wa bunge la vijana kaunti ya Kilifi Jacinta Mbeyu Sanga anasema baadhi ya watoto wa kike wamekosa kupata nafasi za kuboresha maisha yao, hasusan katika masuala ya uongozi kutokana na mila na tamaduni zajadi.

Mbeyu amesema wanawake wengi hupigwa vita katika maswala ya uongozi jambo ambalo, anadai kuwa huchangia pakubwa wao kukosa kufanikisha maono yao.

Wakati huo huo amesema jinsia ya kike imeendelea kudhulumiwa hasa katika masuala ya ajira, kwa madai kuwa wengi hushurutishwa kushiriki ngono ili kupata nafasi za ajira jambo analo amesema linapaswa kuangaziwa na wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

BY EDITORIAL DESK