HabariMazingiraNews

Mabadiliko ya hali ya anga yamechangia mtoto wa kike kutumiwa kama kitega uchumi.

Mabadiliko ya hali ya anga yamechangia mtoto wa kike kutumiwa kama kitega uchumi kwenye baadhi ya familia ambazo zimeathirika na ukame.

Haya ni kulingana na mmoja wa wakaazi wa eneo la Kinango, Mwanasiti Chiliko amedokeza kuwa mtoto wa kike amehusishwa kimapenzi kama njia ya kuleta chakula nyumbani kutokana na kuwa sehemu hiyo hakuna mavuno yoyote yaliyo patakana wakati wa kilimo cha masika.

Aidha mkaazi huyo ametaja umaskini pia kumuathiri mtoto wa kike hali aliyochangia kutohudhuria masomo inavyostahili kwa kukosa vitambaa vya kujihifadhia wakati wa heidh zao.

BY EDITORIAL DESK