Spika wa bunge la kitaifa ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kuwahoji mawaziri walioteuliwa Moses Wetangaula, amesema kuwa uteuzi wa Musalia Mudavadi kuwa Waziri mwenye mamlaka mengi ulizingatia sheria.
Akijibu swali lililoibuliwa na kiongozi wa wachache Opiyo Wandayi ambaye alitilia shaka uhalali wa kumhoji Mudavadi ambaye kwa mtazamo wake si Waziri wa kawaida, Wetangula amesema tofauti ya jina la cheo cha mtu anayetuliwa kuhudumu katika baraza la mawaziri haipaswi kutumika kuharamisha uteuzi wenyewe.
Akiwa mbele ya kamati ya uteuzi Mudavadi amesema kuwa serikali inafaa kupunguza viwango vya deni la kibiashara.
Aidha Mudavadi amesema kuwa serikali bado itakopa lakini kwa busara ili kukopa kusiathiri ustawi wa kifedha wa nchi.
Vile vile amesema kuwa serikali inafaa ilipe madeni yake kwa wakati ufaao.
BY EDITORIAL DESK