Baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Mombasa wamesisitiza haja ya serikali kuhusisha umma kabla ya kuongeza ushuru huku wakidai kuna baadhi ya mabwanyenye serikalini wanakwepa kulipa ushuru.
Wakaazi hao wameitaka serikali kuangazia maoni ya umma kabla kufanya mabadiliko katika utoaji ushuru.
Wakiongozwa na James Maingi Wamesema kuwa kupandishwa kwa ushuru kutawakandamiza wananchi zaidi wakati ambapo mfumuko wa bei za bidhaa muhimu umezidi kupanda.
Aidha wamelaumu serikali kwa kile wamekitaja kukosa usawa katika utoaji ushuru wakidai baadhi ya mabwanyenye na viongozi wakuu serikalini wanakosa kulipa ushuru.
Haya yanajiri siku moja tu baada ya viongozi wa upinzani Raila Odinga na Kalonzo Musyoka kuitaka serikali kuhusisha umma kabla kuongeza utoaji ushuru.
BY EDITORIAL DESK.