Halmashauri ya kuthibiti utendakazi wa kampuni za bima nchini IRA imeanzisha zoezi la kuwahamasisha wafanyibiashara wa sekta ya uchukuzi kuhusiana na uwekezaji kwa bima zilizoidhinishwa na serikali ili ziwafaidi.
Evans kibagendi afisaa wa halmashauri hio amesema kwamba uekezaji katika kampuni za bima ni njiamojawapo ya wafanyibiashara kujiinua kimapato sawia na kuhakikisha usalama wa mali na maisha yao kwa ujumla.
Kibagendi amedokeza kuwa halmashauri hio imeweza kuzifunga zaidi ya kampuni 3 za bima nchini zilizo kuwa zikinyanyasa wateja wao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa muungano wa wahudumu wa matatu Kwale Joseph Mutunga ameafiki wanachama wake kupitia changamoto nyingi za kimsingi kufuatia ukosefu wa kuekeza katika kampuni za bima.
BY EDITORIAL TEAM