Idadi ya maambukizi ya ugonjwa wa malaria umepungua katika kaunti ya Kwale licha ya kuwa uognjwa huo bado ni sugu katika jamii.
Haya yanajiri huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya kimataifa ya malaria.
Kulingana na afisa wa afya katika kitengo cha malaria kaunti ya Kwale Elizabeth Chomba ni kuwa kwa sasa maambukizi ya malaria yanaripotiwa kwa watu 6 kati ya 100 kinyume na miaka ya nyumba ambapo maambukizi ya uginjwa huo yaliripotiwa kwa watu 8 kati ya 100.
Chomba akisema kuwa miongoni mwa mambo yaliyochangia idadi hiyo kupunguwa ni utumizi wa vyandarua vya kujingika na mbu.
Akiongeza kuwa kai ya watu 10 watu 7 wanalala katika neti zilizotibiwa huku idadi ya waliosalia wakiwa hawajatilia maanani umuhimu wa neti za mbu.
BY EDITORIAL DESK