Wizara ya afya kaunti ya kwale imewataka wakaazi hususan wale wanaotumia maji ya vidimbwi kuchukua tahadhari ya mkurupuko wa ugonjwa wa kipindupindu na homa ya matumbo (typhoid) msimu huu wa mvua.
Kulingana waziri wa afya Francis Gwama wakaazi waotumia maji ya mabwawa na visima wamo katika hatari kubwa baada ya maji hayo kuchanganyika na mirudiko ya uchafu unaobeba viini vinavyosababisha na maradhi hayo ambayo mara nyingi husababisha vifo kwa wenyeji .
Amewataka wakaazi hao kuzuru katika vituo vya afya wapate dawa za kutibu maji ili kunusuru maisha yao sawia na kuzingatia maswala ya usafi.