Huenda soko la samaki ulimwenguni likasambaratika endapo mataifa hayataafikia kwa pamoja mikakati ya kuzuia uchafuzi wa mazingira ya bahari kufikia mwaka 2050 .
Kulingana na utafiti uliofanywa na taasisi ya Utafiti wa Afya na Mazingira – Kenya (HERI Kenya) uchafuzi wa mazingira kupitia uchafu wa plastiki umekuwa na athari kubwa kwa viumbe vya bahari na binaadam.
Mwenyekiti wa taasisi hio Francis Mutuku bahari imekuwa na mchango mkubwa kiuchumi wa mataifa kupitia utalii hivyo kusema kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuondoa utumizi wa plastiki hususan chupa ambazo hutupwa ovyo katika fuo za bahari.
Haya yanajiri wakati wa uzinduzi wa sea change plastic planet sculpture ( roboti la mwigo wa mawimbi lililotegezwa na chupa za plastiki )eneo la Diani na taasisi ya utafiti wa afya na Mazingira kenya ..
Roboti hilo likutumika kuikumbusha jamii dhidi ya kutupa ovyo takataka za plastiki katika fuo za bahari badala yake wahifadhi chupa hizo ili kuziuza kwa kampuni zinazotumia taka hizo kutengeza bidhaa tofautitofauti.