HabariNewsSiasa

Bunge la kitaifa lapitisha mswada wa fedha mwaka 2023.

Wabunge katika bunge la kitaifa wamepiga kura kuupitisha mswada tata wa kifedha wa mwaka 2023.

Wabunge 176 wamepiga kura ya ‘ndio’ huku wabunge 81 pekee katika bunge hilo wakipiga kura ya ‘La’.

Matokeo ya kura hizo yamejiri  licha ya vuta nikuvute na pingamizi kutoka kwakwa baadhi ya wabunge hususan wale wanaoegemea mrengo  wa Azimio la Umoja ambao walipinga ripoti hiyo iliyofanyia marekebisho baadhi ya vipengele tata vya mswada huo.

Akitangaza matokeo hayo ya kura Spika wa bunge hilo la Kitaifa Moses Masika Wetangula ameapongeza wabunge wote kwa kushiriki mjadala wa mswada huo.

Mswada huo ambao umesomwa kwa mara ya 2 na kupitishwa, sasa utawasilishwa bungeni tena kusomwa mara ya 3 na kupigiwa kura ya mwisho ya kuupitisha kuwa sheria au kuuangusha.