Ni afueni kwa Serikali Mahakama ikiondoa kwa muda agizo la kusimamisha utekelezwaji wa Sheria tata ya Fedha ya Mwaka 2023.
Mahakama ya Rufaa imeondoa agizo hilo lililotolewa mwezi uliopita na mahakama kuu baada ya serikali kupitia Waziri wa Fedha Njuguna Ndung’u kuwasilisha kesi ikisema kuwa serikali imekuwa ikipoteza fedha.
Waziri Ndung’u kupitia Mwanasheria Mkuu Justin Muturi aliwasilisha rufaa mahakamani akisema kuwa serikali itapoteza bilioni 211 katika mwaka huu wa kifedha kwa kuendelea kusitishwa kutekelezwa kwa sheria hiyo.
Jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji Mohammed Warsame, Kathurima M’inoti na Hellen Omondo wamesema kesi hiyo ya rufaa itasikilizwa na kuamuliwa ndani ya limetoa uamuzi huo unaoipa serikali afueni ya muda huku kesi hiyo ikisubiri kusikilizwa na kuamuliwa ndani ya siku 60.
Katika kile kinachoonekana ushindi wa muda tu kwa serikali ya Kenya Kwanza, Mahakama hiyo imeshikilia kuwa utekelezaji wa sheria hiyo ni kwa manufaa ya umma na kuendelea kusimamishwa.
Hata hivyo Majaji watatu waliosikiliza kesi hiyo ya wakiongozwa na Jaji Mohammed Warsame, Kathurima M’inoti na Hellen Omondo wamesema kesi hiyo ya rufaa itasikilizwa na kuamuliwa ndani ya siku 60.
Haya yanajiri siku chache baada ya Seneta wa Busia Okiya Omtatah kuwasilisha stakabadhi za kurasa 2,065 zinazotoa maelezo zaidi kuhusu kesi yake ya kupinga mswada wa fedha wa mwaka 2023.
BY EDITORIAL DESK