HabariMombasaNews

Serikali yatakiwa kubuni vitengo maalum vya kuangamiza dawa za kulevya.

Serikali imetakiwa kubuni vitengo maalum vya watu wenye ufahamu wa kina kuhusu dawa za kulevya nchini.

Mkurugenzi wa taasisi ya kurekebisha tabia kwa waraibu wa mihadarati ya Reach Out Rehabiliitation Centre kaunti ya Mombasa Taib Abdulrahman, amesema ni sharti kwa serikali kuwezesha wadau mbalimbali wanaousika na vitengo vya kupunguza utumizi wa dawa za kulevya ili taifa lifanikiwe dhidi ya vita hivyo.

Aidha ameipa changamoto serilkali kuhakikisha ufisadi unakabiliwa vilivyo nchini ili kumaliza visa vya dawa za kulevya kusafirishwa kutoka eneo moja hadi lingine.

“Ni lazima kuwa na vitengo vile ambavyo vinafanyia kazi na watu ambao wako na tajriba na wana ufahamu wa kuweza kufanya kazi kama hiyo wawe katika ofisi ambazo zinawapatia nguvu na uwezo wa kutekeleza majukumu yao. Lakini ikiwa tuko na maafisa ambao hawana tajriba ya hali ya juu na ufisadi umekithiri, itakuwa ni vigumu sana kufanya kazi kama hii.”

Haya yanajiri baada ya mahakama ya Malindi kutetekeza  bangi na dawa nyingine za kulevya zenye thamani ya shilingi milioni 25.6.

BY EDITORIAL DESK